Jumatatu , 4th Apr , 2016

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ametembelea daraja la Mto Koga linalounganisha Mkoa wa Tabora na Katavi, na kuagiza wataalamu kulifanyia uchunguzi daraja hilo kabla ya kulifungua baada ya kuharibika na mvua zinazoendele

Mbunge wa Mvomero Sadick Murad akimwongoza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa pili kulia) kuelekea katika daraja la Diwale,

Prof. Mbarawa ametoa agizo hilo Mjini Mpanda na kusema kuwa barabara hiyo itaanza kujengwa hivi karibuni ambapo amewataka wakandarasi kulichunguza daraja hilo kwa kina kabla kuruhusu magari makubwa kuanza kupita.

Prof. Mbarawa ameongeza kuwa haiwezekani kufungua barabara ambayo inaunganisha mikoa bila kufanya uchunguzi kwa sababu kufanya hivyo ni kuhatarisha maisha ya wasafiri na wakazi wanaotumia daraja hilo kubwa kama kiunganisha cha mikoa hiyo katika nyanja zote.

Katika hatua nyingine waziri Mbarawa amesema serikali ipo katika hatua za mwisho za ujenzi wa barabara ya Mpanda mpaka Tabora kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilometa 356 ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyotoa rais Dkt. John Magufuli wakati wa kampeni.

Prof. Mbarawa ametoa kauli hiyo wilayani Sikonge mkoani Tabora mara baada ya kukagua barabara hiyo ambapo pamoja na mambo mengine amesema ujenzi huo unatarajiwa kuanza rasmi ifikapo mwezi june mwaka huu.

Aidha Prof. Mbarawa amesisitiza wananchi wote ambao ujenzi huo utagusa maeneo yao watalipwa fidia kwa mujibu wa sheria hivyo kuwataka kukubali kuondoka mara moja pindi taratibu zitakapokamilika.