Jumatano , 10th Feb , 2016

Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harisson Mwakyembe amesema Mahakama itaimarisha miundombinu yake na kuboresha utoaji wa haki kwa Wananchi baaada ya kupatiwa shilingi sh. Bilioni 12.3 na rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harisson Mwakyembe

Akizungumza jana Jijini Dar es Salaam Dkt. Mwakyembe amesema fedha zilizotolewa zitatatua changamoto kubwa ya kuimarisha miundombinu ya mahakama nchini hasa katika utoaji haki.

Dkt. Mwakyembe amesema kuwa wananchi wanahitaji kupata haki kwa wakati lakini kutokana na changamoto ya miundombinu mibovu inakuwa ni vigumu kulitekeleza jambo hilo kama linavyotakikana.

Kwa upande wake Waziri wa fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amesema Fedha hizo zimeshaingizwa kwenye akaunti ya mahakama tayari kwa matumizi yao.