Jumatatu , 30th Mei , 2022

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, amesema kuanzia leo Mei 30, 2022, serikali imeruhusu magari kupita katika barabara ya juu (Flyover) ya makutano ya barabara ya Chang'ombe na Nyerere jijini Dar es Salaam.

Gari la Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, likipita kwenye Flyover ya Chang'ombe

Akizungumza mara baada ya kutembelea eneo hilo Profesa Mbarawa amesema kuanza kutumika kwa barabara hiyo kutapunguza msongamano wa magari ambao umekuwa ukijitokeza na kuleta usumbufu kwa wananchi

Aidha Profesa Mbarawa, ameagiza hadi kufikia Oktoba mwaka huu barabara zote mbili za flyover katika eneo hilo ziwe zimekamilika na kuanza kutumika mara moja, ambapo hii leo ni upande mmoja tu ndiyo umeanza kutumika, lengo kubwa ni kupunguza msongamano wa magari katika eneo hilo.