Jumatatu , 23rd Aug , 2021

Leo Agosti 23, 2021, Mbunge wa jimbo la Kawe Askofu Josephat Gwajima, atafikishwa mbele ya kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa ajili ya kujibu tuhuma mbalimbali zinazomkabili.

Mbunge wa jimbo la Kawe Askofu Josephat Gwajima

Akizungumza hapo jana kanisani kwake, Askofu Gwajima alisema kwamba akifika kwenye kamati hiyo atasimamia ukweli kama ambavyo imani yake inamtuma.

Licha ya Spika Ndugai kutoa taarifa hiyo, lakini hakuweka bayana tuhuma hizo mbalimbali zinazomkabili Askofu Josephat Gwajima.