Kundi la kutetea haki za binadamu limeongeza kuwa hatua zote zinazochukuliwa kuponda uhuru wa mahakama zinapaswa kubadilishwa.
Ripoti ya hivi karibuni ya shirika hilo iliyochapishwa Jumatatu, ilikuja baada ya Wizara ya Sheria iliyoteuliwa na Saied kukataa kuwarejesha kazini mahakimu 49, licha ya amri ya mahakama ya utawala kufanya hivyo.
Shirika hilo la kutetea haki za binadamu limeelezea kampeni iliyotangazwa na Saied ya kupambana na ufisadi kama unyakuzi wa madaraka ulioanza Julai 25, 2021, wakati Saied alipomfukuza waziri mkuu wa wakati huo Hichem Mechichi na kujipa mamlaka makubwa.
Mnamo Februari 6, 2022,rais huyo alivunja Baraza Kuu la Mahakama (HJC) chombo cha kikatiba kilichopewa mamlaka ya kuhakikisha uhuru wa mahakama na kuibadilisha na baraza la muda kuteua wajumbe wote 21







