Jumatatu , 14th Sep , 2015

Chama cha mapinduzi CCM leo kimezindua kampeni zake za mgombea urais kupitia chama hicho Dkt. Ally Mohamed shein ambapo wametangaza kupata ushindi wa kishindo kupitia umoja wao.

Rais Kikwete, mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM ambaye ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana wakiwa na furaha katika Uwanja wa Demokrasia wa Kibanda Maiti mjini Unguja na kumwaga vipeperushi wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za chama hicho tawala za kugombea Urais wa Zanzibar Jumapili Septemba 13, 2015

Akizungumza katika uwanja wa Demokrasia mara baada ya kukabidhiwa ilani ya Chama cha Mapinduzi amesema kuwa moja kati vitu atakavyoviendeleza ni Amani na Utulivu visiwani humo ambayo mpaka sasa wamefanikiwa kuimrisha kwa kiasi kikubwa.

Dkt. Shein ameongeza kuwa sera kuu ni kujenga umoja wa kitaifa utakaowaunganisha wazanzibari na watanzania kwa ujumla huku akibainisha kuwa bila kuwa na mshikamano nchi haitapata maendeleo.

Akizungumza kabla ya kumkaribisha na kumkabidhi ilani ya CCM mgombea urais wa chama hicho mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho kikwete amesema wana imani kubwa ya kushinda uchaguzi huo.

Aidha Rais Kikwete amesema moja kati ya mambo makubwa ambayo yalikuwa yanaleta utata yameshalimaliza ambalo ni suala la mafuta na kusema kuwa serikali ya mapinduzi kwa sasa itakuwa na mamlaka kamili ya kusimamia suala la gesi na mafuta visiwani humo.