Jumamosi , 8th Aug , 2015

Rais Jakaya Mrisho Kikwete mesema kuwa hakuna mtanzania aliyewahi kufa njaa kwani nchi haikuwahi kuwa na upungufu wa chakula na kusababisha hali ya kuleta athari za kifo kutokana na njaa kwa wananchi wake.

Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa Kilimo akiangalia ndizi iliyolimwa kwa kuzingatia kanuni bora katika shamba

Dkt. Kikwete ameyasema hayo leo mjini Lindi wakati akiwahutubia watanzania katika maadhimisho ya kitaifa ya sikukuu ya wakulima nanenane yaliyofanyika mkoani humo

Dkt. Kikwete amesema kinachofanyika sasa ni kuhakikisha wakulima wanalima mazao mengi zaidi ikiwa ni pamoja na kuwatafuta masoko zaidi na ndani na nje ya nchi ili kuendeleza sekta ya kilomo kwa kukuza uchumi na kuwaondolewa watanzania Umasikini.

Amongeza kuwa licha ya Uzalishaji kuongezeka lakini bado Serikali haijafika inapopataka hivyo haina bundi kuongeza juhudi zaidi ili kuendelea sekta ya kilomo iwe yenye tija zaidi.

Katika maadhimisho hayo Dkt. Kikwete ametumia nafasi yake kuwaaga wakulima ikiwa ni siku chache kabla ya kumaliza muda wake mdarakani, huku akiwataka watanzania kutumia vyema haki yao ya kupiga kura na kumchagua kiongozi wanaompenda.