Jumatano , 20th Apr , 2016

Kufuatia kuongezeka kwa matukio ya Uhalifu wa kutumia Silaha wilayani Kahama mkoani Shinyanga Serikali imeziagiza serikali za vijiji kuanza kutekeleza mpango wa kuorodhesha wageni wanaoingia katika sehemu mbalimbali za wilaya hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Bw. Vita Kawawa,

Akizungumza na baadhi ya viongozi wa halmashauri kuu ya wilaya ya Kahama, Mkuu wa Wilaya ya Kahama Bw. Vita Kawawa, amesema matukio ya uhalifu yalitokea hivi karibuni wilayani humo yamebainika kufanywa na wageni kutoka nchi jirani.

Bw. Kawawa amesema kuwa wageni hao ni lazima wanafikia kwa wananchi ambao ni raia wa Tanzania hivyo wananchi wanawafahamu fika wageni hao hivyo hakuna budi kushirikiana nao ili kuwatambua wageni hao.

Mkuu huyo wa Wilaya amesema baadhi ya wageni hao wamekua wakijihusisha na shughuli mbalimbali ikiwemo za kilimo lakini kuna baadhi yao ambao sio wema wamekua wakifanya matukio ya uhalifu wa kutumia silaha na kufanya mauaji wilayani humo.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama Bw. Vita Kawawa,