
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi.
agizo la Mkuu huyo wa Mkoa.
Uamuzi huo umetolewa na Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa, Patrick Ole Sosopi wakati akizungumza na www.eatv.tv juu ya kiongozi wao kuhitajika kuripoti Iringa kwaajili ya kujibu tuhuma hizo kwa Mkuu wa Polisi, Juma Bwire.
Sosopi amesema, "tunachokifanya kwa sasa ni kufuatilia kama ile 'tweet' ni ya Mkuu wa Mkoa Hapi, lakini sisi hatuwezi kumtoa Katibu wetu Dar es salaam na kumpeleka Iringa wakati sio mwananchi wake, lakini sisi tutakula naye sahani moja."
"Haiwezekani kabisa Katibu wetu atoke Dar aende Iringa, na kuhusu Hilda kuwa na hofu nikwambie kwa sasa haofii chochote, kwa sababu hakuna kosa lolote alilofanya," ameongeza Sosopi.
Mapema mwezi huu Katibu huyo wa BAVICHA Wilaya ya Temeke aliandika ujumbe ambao ulielezea kuwa Ally Hapi aliwahi kujikuta kwenye mazingira ya tofauti ya kulazwa makaburini wakati alilala nyumbani kwake usiku.
Kupitia akaunti ya twitter iliyosomeka kuwa jina la, Ally Salum Hapi, aliagiza kiongozi huyo wa BAVICHA kujisalmisha kwa kamanda wa polisi wa Mkoa wa Iringa kabla ya disemba 21, mwaka huu ili kutoa maelezo.