
Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Doroth Gwajima
Waziri Dkt. Doroth Gwajima ametoa maagizo hayo leo katika mkutano wa wadau wa huduma za ustawi wa jamii jijini Dar es Saaam huku akiomba ushirikiano zaidi kutoka Jeshi la Polisi na Mahakama.
Aidha Waziri Gwajima amewataka watu kutafuta utaratibu mzuri wa kuwasaidia watu wenye uhitaji, na si barabarani wanapoomba, jambo litakalopunguza ombaomba katika majiji na miji mbalimbali nchini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya jamii Bi Zainab Chaula ameeleza kuwa kamati maalumu ya watu 10 iliundwa kutafuta namna ya kupunguza changamoto ya watoto wa mitaani.
Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam amebainisha kuwa kwa Wizara hii kutengwa kutoka Wizara ya Afya itawasaidia maafisa ustawi wa jamii kuyatambua majukumu yao, huku pia akieleza kuwa kwa sasa wamejipanga kuwapeleka katika kambi maalum watoto wa mitaani na omba omba jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wao wadau wa ustawi wa jamii kutoka shirika la Pact Tanzania wameiomba katika mapato ya kila Halmashauri kutenga asilimia 3 ya mapato yake itakayowasaidia maafisa ustawi wa jamii kutekeleza majukumu yao
Mkutano huu umeenda sambamba na uzinduzi wa Miongozo miwili itakayosaidia katika kupunguza ukatili na unyanyasaji kwa watoto, iliyopewa jina la Kanuni za maadili ya kumhudumia mtoto.