Jumanne , 10th Mei , 2016

Serikali imesema kamwe haitamvumilia askari yeyote Yule wa JWTZ anayefanya vitendo vya unyanyasaji wa raia na itaendelea kuwachukulia hatua kadri wanapobainika.

Waziri wa ulinzi na Jeshi la kujenga taifa Dr.Husein Mwinyi.

Waziri wa ulinzi na Jeshi la kujenga taifa Dr.Husein Mwinyi amesema hayo bungeni mkoani Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu mara baada ya kuulizwa hatua anazochukua kwa askari ambao wamekuwa wakifanya vitendo vya unyanyasaji kwa raia.

Dr.Mwinyi amewataka wabunge kuwafichua askari wa JWTZ ambao wamekuwa wakifanya vitendo hivyo vinavyolidhalilisha jeshi hilo ili kulinda hadhi na heshima ya jeshi hilo.

Katika hatua nyingine Waziri Dr.Mwinyi amewasilisha bajeti ya wizara yake na kusema kuwa imedhamiria kulifanya Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania kuwa la kisasa na kutatua kero mbalimbali ambazo zinawakabili askari wake.