Alhamisi , 8th Aug , 2019

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amewasimamisha kazi watumishi 183 wa wizara hiyo kuanzia jana Agosti 7, 2019, ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakbali.

Waziri wa Ardhi William Lukuvi

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Ardhi imezitaja tuhuma hizo kuwa ni kuingilia mfumo wa kukadiria na kukusanya kodi ya pango ya ardhi na kusababisha upotevu wa mapato ya Serikali.

Mbali na kuwasimamisha wafanyakazi hao, Waziri Lukuvi, amemwelekeza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, kuyapeleka majina hayo kwa Mkurugenzi wa TAKUKURU ili uchunguzi uanze mara moja.
 

Majina kamili kama yanavyoonekana hapo chini