Ijumaa , 10th Sep , 2021

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amewaagiza Waziri wa Katiba, Prof.Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mawasiliano Dkt.Faustine Ndugulile, Waziri wa Mambo ya Ndani George Simbachawene, kuhakikisha wanatumia kanuni na sheria zilizopo kuhakikisha vitendo vya matumizi mabaya ya mitandao yanadhibitiwa.

Kushoto ni Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile, na kulia ni Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Septemba 10, 2021, wakati akitoa Hotuba ya kuahirisha vikao vya Bunge hilo hadi Novemba 2, 2021, ambapo amesema kuwa siku za hivi karibuni watu wameanza kutumia vibaya mitandao ya kijamii kwa kutoa taarifa za upotoshaji na zenye kudhalilisha.

"Katika kulinda na kutunza usalama, amani, umoja na mshikamano wa nchi ninawaagiza Waziri wa Katiba na Sheria, Waziri wa Mambo ya Ndani, Waziri wa Mambo ya Nje, Waziri wa Utumishi, Waziri wa Mawasiliano na Teknolojiana ya Habari kutumia sheria, kanuni na taratibu zilizopo kuhakikisha vitendo vya matumizi mabaya ya mitandao vinadhibitiwa hapa nchini," ameagiza Waziri Mkuu.