Mtaalam ataja dawa ya nguvu za kiume

Jumatano , 15th Jan , 2020

Mtaalam wa masuala ya Lishe kutoka Taasisi ya Mifupa Kitengo cha Muhimbili Zainab Tindi amesema moja ya suluhisho kubwa kwa wanaume wenye tatizo la nguvu za kiume ni kufanya mazoezi.

Tindi ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye kipindi cha Supa Breakfast cha East Africa Radio, kinaruka kila siku Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 12 : 00 asubuhi hadi Saa 4 asubuhi.

Tindi amesema kuwa "wanaume wengi siku hizi utasikia wanalalamikia nguvu za kiume, fanyeni mazoezi yatawasaidia" 

Aidha amesema kuwa "mazoezi hutibu mishipa ya nguvu za kiume, na kudhibiti uzito mtiririko wa damu kwenye sehemu za uzazi za wanaume hata wanawake hivyo huongeza ujasiri "