Alhamisi , 3rd Mar , 2016

Wafugaji jamii ya wamasai wanaoishi katika kijiji cha visakazi wilaya ya Chalinze mkoani Pwani wamekuwa na hofu ya kupeleka mifugo yao katika eneo walilotengewa na serikali kutokana na eneo hilo kuvamiwa na wakulima kinyume na utaratibu.

Wafugaji wakiwa katika moja ya Mashmba ya malisho

Wakizungumza mbele ya uongozi wa kijiji hicho wafugaji hao wamesema hivi sasa wamechoka kuonekana kuwa wao ndio chanzo cha migogoro ya wakulima na wafugaji na kwamba ili waweze kuwa huru na shughuli za ufugaji serikali iwaondoe watu wote waliovamia eneo hilo la malisho ambaapo mbali na kuwepo mashamba wengine wameweka makazi ya kudumu

Wakijibu malalamiko ya wafugaji hao mjumbe wa serikali ya kijiji hicho cha Visakazi Bi. Semeni Khamisi pamoja na Salum Bafta wameweka bayana juu ya uvamizi wa eneo hilo na kueleza kuwa uongozi hauhusiki kabisa na jambo hilo na kuomba ngazi za juu kuingilia kati tatizo hilo

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji hicho bw. Moses Mghwira amesema tayari hatua zimeanza kuchukuliwa dhidi ya watu wote waliovamia maeneo ya wafugaji pamoja na maeneo oevu hali itakayosaidia kuepusha migogoro isiyo ya lazima katika kijiji hicho.

Hatahivyo mkutano huo nusura uvunjike kutokana na baadhi ya wafugaji pamoja na wajumbe wa serikali ya kijiji kuonyesha jaziba na kuutuhumu uongozi wa kijiji kuhusika na suala la kuuza maeneo ya wafugaji