
Wengine kadhaa walijeruhiwa katika shambulio la Alhamisi, Mahdi al-Mashat ameongeza bila kutoa maelezo. Katika taarifa yake ya ijumaa, Israel ilisema kuwa shambulio hilo la anga lilimlenga mkuu wa majeshi wa kundi linalofungamana na Iran, waziri wa ulinzi na maafisa wengine wakuu.
Ahmad Ghaleb al-Rahwi aliteuliwa kuwa waziri mkuu mwaka mmoja uliopita, lakini kiongozi mkuu wa serikali alikuwa naibu wake, Mohammed Miftah, ambaye aliteuliwa Jumamosi kutekeleza majukumu ya waziri mkuu. Rahwi alionekana kwa kiasi kikubwa kama mtu maarufu ambaye hakuwa sehemu ya ndani ya uongozi wa Houthi.
Alikuwa mshirika wa Rais wa zamani wa Yemen Ali Abdullah Saleh, ambaye Wahouthi walimtimua kutoka Sanaa mwishoni mwa 2014 na kusababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa muongo mmoja, lakini baadaye wakaungana na kundi hilo. Yemen imegawanyika kati ya utawala wa Houthi huko Sanaa na serikali inayoungwa mkono na Saudia huko Aden tangu wakati huo.
Tangu vita vya Israel huko Gaza dhidi ya kundi la wanamgambo wa Palestina Hamas kuanza Oktoba 2023, Wahouthi wanaoungwa mkono na Iran wameshambulia meli katika Bahari Nyekundu kwa kile wanachoeleza kuwa ni vitendo vya mshikamano na Wapalestina.
Pia mara kwa mara wamerusha makombora kuelekea Israel, ambayo mengi yamezuiliwa. Israel imejibu mapigo kwa maeneo yanayodhibitiwa na Wahouthi nchini Yemen, ikiwemo bandari muhimu ya Hodeidah.
Waziri wa Ulinzi wa Israel Israel Katz alisema jana Jumamosi kwamba shambulio hilo lilikuwa ni"pigo kubwa" dhidi ya WaHouth, akiongeza kuwa huu ni mwanzo tu.