Jafo awataka WaTZ kuiombea nchi

Jumatatu , 12th Aug , 2019

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Selemani Jafo, amewataka Watanzania kuungana pamoja na kuendelea kuliombea taifa na kumuomba Mungu, atuepushe na majanga kama yanayojitokeza kwa sasa.

Waziri Jafo amebainisha wakati wa swala ya Eid- El - Adh'aa, iliyofanyika katika viwanja vya Masjid Kibaden Ilala Dar es salaam, ambapo ametumia nafasi hiyo kuwaomba watanzania, kuwaombea waliotangulia mbele za haki.

"Janga hili la juzi linatukumbusha janga lililotokea katika Kijiji cha Isongore Mkoani Mbeya miaka ya nyuma, lilitokea na watu wengi walipoteza maisha, janga kama hili si Tanzania pekee, sehemu nyingine kama Ghana, Nigeria, Congo limeshawahi kutokea" amesema Waziri Jafo.

Waziri Jafo amesisitiza kuendelea kufanya maombi makubwa kwa Tanzania.