
Kiongozi huyo wa Chama cha Liberal Democratic Party (LDP), mwenye umri wa miaka 64, ameshinda katika uchaguzi uliofanyika ikiwa ni jaribio lake la tatu la kuwa Waziri Mkuu.
Aidha kura iliyomchagua Takaichi, haikuwa ya watu wote nchini humo, bali ilipigwa na wabunge katika Bunge la taifa hilo, ni aina ya siasa inayochagua kiongozi kati yao Wabunge wenyewe.