Jumamosi , 25th Jul , 2020

Jeshi la Polisi Nchini limetoa onyo kali kwa viongozi wanaohamasisha mikusanyiko ya watu isiyo zingatia sheria za nchi na yenye lengo ovu kwa taifa.

Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini (SACP) David Misime

Kauli hii imetolewa leo Julai 25, 2020 kufuatia kuwepo kwa baadhi ya viongozi wa CHADEMA wanaohamasisha watu kupitia mitandao ya kijamii kukusanyika kwenda kumpokea mmoja wa wanachama wao (taarifa haijamtaja) anayetarajia kuwasili nchini Tanzania kwenye uwanaja wa Mwl. Nyerere Julai 07, 2020.

Jeshi la polisi limesema linatambua watanzani wapo kwenye kipindi cha maombolezo lakini hilo halitawazuia kuwawajibisha kwa mujibu wa sheria wale wote wanaokusudia kufanya mikusanyiko bila kuzingatia sheria.

Soma taarifa kamili ya Polisi.