
Rais Magufuli akiwa na IGP, Simon Sirro.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Desemba 21, 2018 katika mahafali ya kuhitimisha mafunzo ya Maofisa na Wakaguzi Wasaidizi wa Polisi, ambapo amesema kuna baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakilituhumu jeshi hilo kwa vitu ambavyo, amedai si vya kweli.
"Mwaka 2019 tunaingia katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, nawaomba Jeshi la Polisi mkasimamie nidhamu," amesema Rais Magufuli.
Ameongeza kuwa, "Watu wasioukuwa na shukrani ndio watawasema vibaya, lakini sisi tunaotambua na kuthamini mchango wenu katika ulinzi wa taifa hili, tunatembea kifua mbele huu ni ukweli usiofichika kuwa Jeshi la Polisi mnafanya kazi nzuri".
Kwa upande wake, Inspekta Jenerali wa Polisi, IGP Simon Sirro amesema Jeshi hilo limejipanga vya kutosha kusimamia usalama katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2019 na uchaguzi mkuu wa 2020, na kusema kuwa hawatatoa nafasi kwa mtu yeyote atakayehatarisha amani ya nchi.
Katika hafla hiyo ya mahafali, jumla ya wahitimu 513 wamemaliza kozi ya maofisa polisi na wakaguzi wasaidizi.