
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, David Kafulila
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, David Kafulila, amefikia uamuzi wa kuzuia shughuli ya uchimbaji wa dhahabu katika duara hizo, baada ya kupokea malalamiko ambapo amemuomba Waziri wa Madini, Dotto Biteko, kutuma wataalamu wake kuja kutoa tafsiri ya mgogoro huo wa kimaslahi.
Hata hivyo, wakati Kafulila akiwa mgodini hapo kusikiliza kero za wachimba madini hao, zikaibuka tuhuma za rushwa, na mkuu wa mkoa akaagiza vyombo vya dola kuwashughulikia wahusika wa vitendo hivyo vya rushwa.