'Kamanda wa TAKUKURU mchukue huyu' - Majaliwa

Jumatatu , 7th Oct , 2019

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemwagiza Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Singida, Bw. Adili Elinipenda amkamate Afisa Manunuzi wa Chuo cha Ualimu Kinampanda, Bw. Francis Muyombo kwa kukiuka taratibu za manunuzi ya Serikali na kughushi nyaraka.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimhoji Afisa Manunuzi wa Chuo cha Ualimu Kinampanda, Bw. Francis Muyombo.

Pia alimwagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, ACP Sweetbert Njewike amkamate na kumhoji Bw. Joseph Kisaka ambaye alikuwa mzabuni wa chuo hicho kwa kuwapatia (kusupply) vifaa ambavyo ni chini ya kiwango.

Ametoa agizo hilo wakati akikagua ukarabati wa majengo ya chuo hicho kilichopo wilayani Iramba, mkoani Singida ambako alibaini delivery note ikionesha kitasa kimoja kimenunuliwa kwa sh. 70,000 badala ya sh. 25,000.

Waziri Mkuu alisema 'quotation' ya manunuzi inaonesha kwamba walipaswa kununua vitasa ambavyo vinafunga mara tatu (vya 3-level) lakini alipokwenda kukagua milango kwenye mabweni, ukumbi, na bwalo alikuta ni vitasa vya kufunga mara moja (vya 1-leavel).

“Serikali imetoa sh. bilioni 1.4 kwa kila chuo ili kufanya ukarabati wa vyuo vya elimu kikiwemo hiki cha kwenu. Ninyi mnanunua vifaa kinyume na utaratibu wa Serikali, hamvikagui, mnaweka tu vitu hafifu ambavyo havidumu. Haiwezekani!”.

Zaidi tazama Video hapo chini