Kamishna Polisi alamba uteuzi wa JPM

Jumapili , 21st Jun , 2020

Rais Magufuli leo, Juni 21, 2020 amefanya uteuzi wa nafasi mbili za Wakuu wa Wilaya.

Rais Magufuli

Amemteua Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jotham Balele kuwa Mkuu wa Wilaya ya Monduli mkoani Arusha, akichukua nafasi ya Idd Kimanta ambaye amaeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Kabla ya uteuzi huo, ACP Balele alikuwa Wizara ya Mambo ya Ndani.

Pia Rais Magufuli amemteua Bw. Bakari Msulwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro mkoani Morogoro, akichukua nafasi ya Bi. Regina Chonjo ambaye amestaafu.

Kabla ya uteuzi, Bw. Msulwa alikuwa Afisa Mwandamizi na Mtangazaji wa TBC.

Wateule hao wanatakiwa kuwepo Ikulu Jijini Dar es Salaam, kesho 22 Juni, 2020 saa 2:30 Asubuhi.