Kampuni ya Icea Lion yaboresha huduma ya bima

Jumamosi , 5th Dec , 2020

Katika kuendelea kuifanya nchi kuwa  ya uchumi wa kati, makundi mbalimbali yakiwemo ya wafanyabiashara, wafanyakazi na wakulima wametakiwa kukata bima ikiwemo bima ya makazi, afya, mazao pamoja na vyombo vya moto ili kujihakikishia usalama wa mali zao.

Mkuu wa wilaya ya Nyamagana,Dkt Phillis Nyimbi

Hayo yamebainishwa jijini Mwanza na Meneja wa bima kanda ya Ziwa Sharif Hamad, kwenye hafla iliyofanywa na kampuni ya bima ya Icea Lion, ambapo makundi hayo yametakiwa kjiunga na bima ili  kuepukana na kununua ama kufanya marekebisho ya mara kwa mara.

Awali akifungua hafla hiyo kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, mkuu wa wilaya ya Nyamagana Dkt Phillis Nyimbi, amesema makundi  mbalimbali yakiwemo ya wafanyabiashara na wakulima yanatakiwa kupewa elimu ya namna ya kukata bima.

Kampuni ya bima ya Icea Lion, imekuwa ikitoa huduma ya bima kama bima ya ujenzi, magari, biashara, safari, usafirishaji, viwanda, vituo vya mafuta bima ya moto kwa nyumba binafsi na viwandani, bima za meli, ndege, wizi na bima nyingine.