Ijumaa , 30th Aug , 2019

Njia za uzazi wa mpango zimekuwa zikitumika sana kwa wadada, wanawake na akina mama nchini, lakini zikitumika bila madhara zinaweza kuleta changamoto ya uzazi kama ambavyo mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini Mh. Patrobas Katambi ameamua kushughulika na tatizo hilo.

Mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini Mh. Patrobas Katambi

Katika mahojiano maalum  na EATV & EA Radio Digital ofisini kwake mjini Dodoma, Katambi amesema kuwa wamegundua uwepo wa tatizo hilo hivyo wamekuja na mpango mkakati kwaajili ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma.

''Kumekuwa na matumizi ya P2 bila kupata vipimo na ushauri wa daktari hivyo kusababisha madhara ya pengine watu kukosa kuolewa au kukosa watoto, lakini sasa tumekuja na huduma ya Mobile ili watu waweze kupimwa na kupata ushauri kutoka kwa wataalamu popote walipo'', - Amesema Katambi.

Aidha Katambi ameeleza kuwa Wilaya yake kwa ujumla imepiga hatua katika masuala ya huduma za Afya, Elimu na ujenzi wa miundombinu ya kisasa katika kile sekta.

Zaidi tazama Video hapo chini.