Kauli ya Lowassa kuhusu uamuzi wa Sumaye

Alhamisi , 5th Dec , 2019

Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, amesema hawezi kusema chochote juu ya hatua alizozichukua Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, kutangaza kukihama Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA na kuwa mshauri wa chama chochote.

Sumaye kizungumza Lowassa

Lowassa ametoa kauli hiyo leo Desemba 5, 2019, wakati akizungumza na EATV na EA Radio Digital, iliyotaka kufahamu juu ya uamuzi wa Sumaye ambapo mwaka 2015 wote wawili, walitangaza uamuzi wa kuhamia chama hicho kwa kile walichokidai, kutokuwepo kwa Demokrasia ndani ya CCM.

Mtangazaji (Sangu Joseph)"Jana Sumaye ametangaza kuhama CHADEMA na kuwa mshauri wa chama chochote, kama mkongwe wa siasa nchini, nini maoni yako katika hili?".

"Kuhusiana na suala hilo kwa sasa mimi siwezi kuzungumza chochote nadhani ungeniacha tu" amejibu Lowassa.

Jana Disemba 4, 2018, wakati akitangaza uamuzi wa kuhama chama hicho, Sumaye alisema sababu kubwa ya kuhama ni kukosekana kwa Demokrasia ya kweli ndani ya chama hicho.

"Baada ya kutafakari kwa kina, ustaarabu unasema toka sasa hutakiwi, wako watakaosikitika nimelazimika kujiondoa CHADEMA kutoka leo hii, mimi sio Mwanachama wa CHADEMA na sijiungi na chama chochote, ila niko tayari kutumika na chama chochote" Alisema Sumaye.