Jumatano , 4th Dec , 2019

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amemwambia Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye uwa alimueleza asingeweza kupata kazi ya kushauri chama chochote cha siasa kama angekuwa nje ya Chama Cha Mapinduzi.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole.

Polepole ametoa kauli hiyi saa chache baada ya Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye kutangaza nia yake kujiondoa ndani ya CHADEMA kwa kile alichokidai kuwa hakuna demokrasia ya kweli.

Polepole ameandika kuwa "Mzee nilikwambia, kazi ya ushauri hutaipata ukiwa nje ya CCM wenzako wanatushauri na tunazingatia ushauri wao kwa sababu tunawaheshimu, ni wana CCM na kiitikadi tuko pamoja.Umebaki bila Itikadi, ile ni mali ya mtu ni yake, nilikwambia mwache, ona sasa unahama mara ya 2"

Akitangaza uamuzi wa kujiondoa CHADEMA Waziri Mkuu Mstaafu Sumaye amesema kuwa "baada ya kutafakari kwa kina, ustaarabu unasema toka sasa hutakiwi, wako watakaosikitika nimelazimika kujiondoa CHADEMA kutoka leo hii, mimi sio Mwanachama wa CHADEMA na sijiungi na chama chochote, ila niko tayari kutumika na chama chochote"