Jumatatu , 13th Jul , 2020

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole, amewaonya wale wote waliokuwa wametengeneza vipeperushi na mabango na kuyaweka mitandaoni ya kwamba wanatangaza nia ya kugombea Ubunge katika jimbo fulani, waache mara moja kwa kuwa wameanza kampeni kabla ya wakati.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole.

Polepole ametoa kauli hiyo hii leo Julai 13, 2020, Jijini Dodoma, wakati akitoa ratiba ya mchakato mzima wa kuwapata wagombea wa nafasi za Ubunge na Uwakilishi kwa upande wa Zanzibar, ambapo amesema kuwa tayari amekwishaona watu wanavyosambaza mabango yao wakijinadi.

"Tumeshaanza kuona watu wanabandika mabango mitandaoni mnatangaza nia, ndugu yangu lile ni kosa, umeanza kampeni kabla ya wakati, kule ni kujipitisha kimtandao kwa wanachama, vipi yule ambaye hawezi kujitangaza kwa mtindo huo, ninawaonya muache mara moja kutumia mabango na vipeperushi kabla ya mchakato wa uchaguzi, fomu zitaanza kuchukuliwa kesho, wewe unaanza kujipiga mabango ni kinyume na taratibu tulizojiwekea" amesema Polepole.