Jumatano , 4th Jan , 2023

Baraza la vyama vya siasa nchini kwa kushirikiana na wenyeviti wa vyama mbalimbali vya siasa, wameeleza kuunga mkono hatua ya Rais Samia ya kuruhusu mikutano ya hadhara na kusema hali hiyo imeonesha ukomavu wa demokrasia iliyopo nchini.

Wenyeviti wa vyama mbalimbali nchini

Akizungumza katika mkutano leo Mwenyekiti wa Chama cha CUF Profesa Ibrahimu Lipumba, amesema katika kipindi cha miaka mingi fursa hiyo haikuweza kupatikana hivyo kuruhusu mikutano hiyo ni sawa na kuwapa fursa wananchi ya kuchambua na kuchagua yale mazuri na mema yaliyopo kwenye vyama hivyo.

Naye mwenyekiti wa baraza la vyama vya siasa nchini Juma Ali Hatibu, amesema wamefurahishwa na umoja wa kisiasa ambao sasa umeanza kuonekana kwa kuwa walikuwa wakikosa amani na furaha pale vyama vya siasa vinapokutana na serikali huku chama kimoja hakipo jambo ambalo sasa Rais Dkt Samia amelishughulikia na kulimaliza kwa kuleta maridhiano

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha ADC Hamad Rashid, amesema vyama hivyo vinakwenda kufanya mikutano hiyo ya hadhara kwa kuzingatia maslahi mapana ya taifa pamoja na kufuata ushauri ambao Rais Dkt Samia ameutoa wa kufanya siasa za kistaarabu.