Jumatano , 23rd Sep , 2020

Mgombea Urais kupitia CHADEMA Tundu Lissu amewaomba wakazi wa Kamachumu mkoani Kagera, wachague mbunge atakayeweza kuwawakilisha vyema wananchi Bungeni na siyo yule aliyewahi kusema kuwa mtu akiwa na cherehani 4 ni kiwanda.

Tundu Lissu, Mgombea Urais kupitia CHADEMA.

Lissu ametoa kauli hiyo leo Septemba 23, 2020, ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake za kufanya mikutano ya kampeni mkoani Kagera.

"Bungeni pelekeni mtu ambaye anajua kuongea, Bunge linaitwa baraza la taifa la kutunga sheria ni pahala pa kuzungumza, msipeleke tena yule jamaa aliyesema ukiwa na cherehani nne wewe una kiwanda", amesema Tundu Lissu.

Aidha Lissu ameongeza kuwa, "Najua tutashinda Muleba Kaskazini na Mkoa wa Kagera sina shaka, nimetembea sana tangu juzi ninajua hali ilivyo, ninawaomba ndugu zangu inabidi tushinde kwa kimbunga, wakute tumeshinda katika kila kituo cha kupigia kura".