Ijumaa , 13th Aug , 2021

Kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, na wenzake imeahirishwa hadi Agosti 27 mwaka huu kwa ajili ya kusikiliza hoja zilizowasilishwa na upande wa washitakiwa kuhusu matamshi yaliyotolewa na taasisi moja ya serikali kuhusu washtakiwa wao.

Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe

Kesi ya hiyo ya uhujumu uchumi leo Agosti 13, 2021 ilikuwa inasikilizwa kwa njia ya mtandao ‘Video Conference’ ambapo yeye Mbowe alikuwa Gereza la Ukonga.