Kigoma: Daktari aua mpenzi wake kwa nyundo

Jumanne , 14th Jan , 2020

Jeshi la Polisi mkoani Kigoma linamshikilia daktari wa Chama cha Msalaba Mwekundu (Red Cross) kambi ya wakimbizi ya Nduta wilayani Kibondo kwa kosa kumuua mpenzi wake kwa kumpiga na nyundo kichwani kisha naye kufanya jaribio la kujiua.

Nyundo

Akielezea tukio hilo kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma, Martin Otieno amesema tukio hilo limetokea Jumapili, Januari 12 ambapo mshtakiwa Albert Rugai (65) alimuua mpenzi wake, Ester Kondo (42) kwa kumpiga kwa nyundo kichwani kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Kwa upande wake mganga mfawidhi Hospitali ya Wilaya ya Kibondo Dr. Martias Bwashi amesema kuwa wamepokea mwili wa marehemu pamoja na mtuhumiwa anayedaiwa kuua, kwa ajili ya matibabu akiwa chini ya uangalizi wa polisi.