Jumanne , 4th Oct , 2022

Vilio na simanzi vimetawala kwa wakazi wa Kata ya Kolandoto, mkoani Shinyanga, baada ya watu wawili kuuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali na kijana anayesadikiwa kuwa na matatizo ya akili na kisha wananchi wenye hasira kumuuwa muuaji huyo kwa kumshambulia kwa mawe na kumchoma moto.

Wananchi wa Kolandoto wakiwa na majonzi kufuatia vifo vya wananchi wenzao

Tukio hilo limetokea jana Oktoba 3, 2022, ambapo baada ya kufanya mauaji hayo kijana huyo pia alijeruhi wengine watatu na yeye kuuawa na wananchi.

Kwa upande wao baadhi ya wakazi wa Kata ya Kolandoto, wamesema tukio hilo limewaacha na simanzi kubwa, kutokana na kupoteza ndugu zao ambao walikuwa ni nguvu kazi ya Taifa, huku Mganga Mkuu wa hospitali ya Kolandoto Dkt.Joseph Wallace, amesema amepokea miili ya watu watatu na majeruhi watatu.

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.