Jumatatu , 14th Oct , 2019

Wakati Watanzania wakiungana kwa pamoja kuazimisha miaka 20 tangu kitokee kifo cha Baba wa Taifa wa Mwalimu Julius Nyerere, moja ya matukio ambayo yanakumbukwa zaidi ni tukio la kupigwa mtama kwa aliyekuwa Msaidizi wa wa RPC wa Mkoa wa Dar es salaam, Alfred Gewe,

ambaye alifahamika kwa ajila la James Kombe.

James Kombe alipigwa mtama na baadhi ya wapiga picha ambao walijitokeza kwenye kushiriki kuupokea mwili wa Hayati Baba wa Taifa, ambapo walikuwa wanapiga picha kwa ajili ya kuzichapisha kwenye vyombo vyao vya habari lakini yeye akawa anawazonga,

Akisimulia kisa hichoa aliyekuwa mpiga picha wa Gazeti la Majira, wakati akihojia na Mtangazaji wa East Africa Radio, Charles William amesema, "Wakati wakupokea mwili wa Baba wa Taifa kulikuwa na Msaidizi wa RPC Dar es salaam Alfred Gewe, aliyejulikana kwa jina la James Kombe, alipigwa mtama na wapiga picha, alikuwa akiwazonga, wasipige picha na kushuhudia mapokezi ya kipenzi cha Watanzania, Nyerere alikuwa kipenzi cha kila mtu."

Mwalimu Julius Nyerere, alikuwa ni miongoni mwa waasisi wa Bara la Afrika ambao waliratibu kupatikana kwa uhuru kwa nchi nyingi zilizopo kusini mwa bara la Afrika kwa kushirikiana na wenzake wakina Nelson Mandela.

Pia Leo Oktoba 14, 2019 ni mwisho wa kujiandikisha kwa wananchi kwenye daftari la mpiga kura, kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.