Wananchi wa kijiji cha Ntinga kata ya Msangano wilayani Momba mkoani Songwe wamelazimika kuyakimbia makazi yao na kutafuta hifadhi katika shule ya Msingi msangano kufuatia mafuriko ya maji yaliyovamia makazi hayo kutokana na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo katika wilaya za Ileje, Mbozi na Tunduma mkoani humo.

