Ijumaa , 11th Oct , 2019

Kuelekea mchezo wa leo wa kalenda ya FIFA ambao pia ni wa kufuzu EURO 2020, kati ya England dhidi ya Jamhuri ya Czech, kocha wa England Gareth Southgate ameeleza sababu za kumwacha Jesse Lingard.

Katika mahojiano aliyofanya Gareth Southgate, amesema ukweli ni kwamba Lingard anapitia wakati mgumu na yeye mwenyewe anajua hilo, hivyo hakuna maajabu yeye kutomuita kwenye kikosi chake.

'Lingard anajua kuwa anapitia wakati mgumu kutokanana na nafasi anayocheza ya kiungo mshambuliaji, unapimwa kwa vitu viwili tu, magoli unayofunga au msaada wa magoli unaotoa na si vinginevyo', amesema.

Southgate ameongeza kuwa kwenye kikosi chake kwa sasa kuna wachezaji wa eneo la kiungo mshambuliaji wengi na wanafanya vizuri na ni vijana pia kama Jadon Sancho, hivyo wanahitaji nafasi zaidi.

UANGALIZI WA UEFA

Kwa upande mwingine Shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA), limeweka wazi kuwa litaweka waangalizi kwenye michezo ya baadhi ya mataifa ili kuhakikisha wanabaini na kukomesha vitendo vya ubaguzi vinavyoonekana kushamili kwenye soka la Ulaya.