Alhamisi , 15th Sep , 2022

Kundi la  tisa la wakazi wenyeji wa eneo la hifadhi ya Ngorongoro limeondoka leo Septemba 15/2022 kuelekea kijiji cha Msomera na kufanya idadi ya kaya zilizohama eneo hilo kufikia 213 zenye Watu 1233 na Mifugo 7442 

Msisitizo umeedelea kuwekwa kwa Jeshi la kujenga Taifa kuongeza kasi ya ujenzi wa nyumba katika kijiji cha Msomera,ili iweze kuendana na kasi ya wanao jiandikisha.

Akitoa taarifa ya Maendeleo ya zoezi hilo kwa msemaji mkuu wa serikali Gerson Msigwa ,naibu kamishna wa uhifadhi NCAA Dkt Christopher Timbuka amesema kwa sasa idadi ya wanao jitokeza kujiandikisha kwa hiari imekuwa maradufu na kuanza kutishia upatikanaji wa nyumba kule Msomera 

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Raymond Mangwala amesema hali ya uhifadhi wa mimea na wanyamapori katika maeneo waliyohama wananchi imeanza kurejea kwa kasi, kwani kwa sasaa inawezekana kuona wanyama wote wakubwa almarufu the BIG FIVE