Ijumaa , 17th Jul , 2015

Kuporomoka kwa uchumi wilayani Kyela Mbeya ndiyo sababu ya wananchi kushindwa kumudu gharama za kuwasomesha watoto mashuleni na kupeleke wilaya hiyo kuwa ya mwisho kwa ufauru katika wilaya tisa za mkoa wa Mbeya.

Mkufunzi wa chuo cha mipango kilichopo mkoani Dodoma Dkt. Lucas Mwambambale ambae ametangaza nia ya kugombea jimbo la kyela.

Kauli hiyo imetolewa na mkufunzi wa chuo cha mipango kilichopo mkoani Dodoma Lucas Mwambambale wakati akitangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Kyela.

Akizungumza na kituo hiki amesema endapo atapata ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na akipita kwenye uchaguzi mkuu atahakikisha anaboresha sekta zote zilizodhorota ikiwemo ya elimu hasa kwa masomo ya Sayansi ambapo ataboresha maabara.

Aidha amesema kuwa' mbali na serikali kuhamasisha wananchi kujenga shule za kata na mahabara lakini hakuna maboresho ikiwa ni pamoja na nyumba za waalimu na maslahi yao ndiyo sababu ya kuyumba kwa elimu wilayani humo huku viongozi waliopo madarakani wakishindwa kunusuru ali hiyo.

Mwambambale ambaye aliwahi kuwa afisa mtendaji mkuu wa mamlaka ya mji mdogo wa Kyela wakati inaanzishwa miaka kadhaa iliyopita amesema anashangazwa kuona bado hawajapata halmashauri ya mji licha ya kukidhi vigezo. Amesema akiwa mbunge atahakikisha wanafanikiwa.