Jonathan Kusi
Jonathan ameyaeleza hayo kupitia mahojiano kwenye kituo kimoja cha runinga na kusema hawezi kusahau namna alivyopoteza kiasi hicho cha pesa ndani ya miezi mitatu, fedha ambazo zingine zilikuwa ni za kukopa.
Jonathan alisema masaibu yake yalianza pale alipopoteza zaidi ya shilingi milioni 233 za Kitanzania katika muda wa miezi 3 na kuamua kuwa atafanya lolote lile ili kurejesha pesa hizo.
Jonathan alipoulizwa kama alishawahi kushinda kupitia kubeti alisema kwamba aliwahi na kuongeza kwamba katika kazi ya kubeti watu wengi hupoteza zaidi fedha kuliko jinsi wanavyoshinda fedha
Akizungumzia namna ambavyo amejidhatiti kulipa madeni ya watu amesema, alijaribu kuuza baadhi ya mali zake ikiwemo gari na nyumba ili aweze kulipa madeni.
Aidha Jonathan pia aliwahi kuwa Meneja Mkuu wa moja ya kampuni nchini kwake.