Lipumba atangaza hatma ya mgombea Urais CUF

Alhamisi , 2nd Jul , 2020

Mwenyekiti wa CUF Taifa, Prof Ibrahim Lipumba amesema kama kuna mwananchama yoyote wa CUF anaedhani ana sifa ya kugombea Urais wa Jahmri ya Muungano wa Tanzania ajitokeze kuchukua fomu bila woge wowote.

Profess Ibrahim Lipumba

Prof. Lipumba ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kama Chama cha wananchi CUF kitapewa ridhaaa, Oktoba 2020 kitajielekeza katika kurejesha Uhuru wa haki za binadamu pamoja na Uhuru wa kujieleza ikiwemo kufuta kwa baadhi ya sheria inazodai ni kandamizi za kimtandao ambazo zimetungwa hivi karibuni.

Amebainisha katika kikao cha Baraza la Kuu la Taifa la chama hicho limefikia maazimio ya kumchagua Bw. Haroub Shamsi kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho.

Kuhusu hamahama ya vyama amesema kwa sasa chama kimeweka mfumo na utaratibu kwa watu kitakaowapa nafasi za kugombea kuanzia nafasi za udiwani.