Maandalizi ya kuagwa Mzee Mkapa uwanja wa Uhuru

Jumamosi , 25th Jul , 2020

Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Abubakari Kunenge amesema taratibu za maandilizi ya kuuaga mwili wa aliyekuwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa yanaendelea kwenye uwanja wa Uhuru pamoja na kuimarishwa kwa hali ya Ulinzi na Usalama.

Maandalizi kwenye uwanja wa Uhuru ambapo atazikwa Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin William Mkapa

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Uwanja wa Uhuru Temeke Jijini Dar Es Salaam amesema 

"Tunashukuru sana kwa mapenzi yenu makubwa kwa viongozi wetu, naamini tutafika kwa wingi na wasioweza kupata nafasi uwanjani tunaomba mkae barabarani tutawapatia ratiba ni njia ipi ambayo mwili utapita hadi kufika hapa ili wote mmpate fursa ya kumuaga huko mlipo" Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Abubakari Kunenge 

"Tunafanya taratibu kujua ni njia gani ambayo atapita pamoja na taratibu zingine ambazo zinafanywa katika ngazi ya Taifa kulingana na itifaki na niwahakikishie wananchi wa Mkoa wa Dar Es Salaam hali ya usalama ni nzuri na tumejipanga vizuri kwa hiyo tusiwe na wasiwasi tujitokeze kwa wingi na kuaga ni kuanzia asubuhi hadi jioni" ameongeza 

Zaidi tazama kwenye video hapo chini.