Jumatano , 15th Jan , 2020

Msanii wa Hiphop nchini Mabeste amemshangaa Msanii mwenzake wa Hiphop Stamina  kwa kile alichokidai kuvujisha siri za Mkewe kwenye video yake mpya ya 'Asiwaze' na kusema yeye hawezi kufanya hivyo.

Mabeste

Mabeste ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye kipindi cha eNewz cha EATV kinachoruka kila siku Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 12: 00 hadi 12 : 30.

Mabeste amesema kuwa "Mimi siwezi kuchanganya mambo ya kawaida yakaja kwenye mziki wangu, unajua ukichukua hali ya faragha kati ya mke na mume ambatyo yalikuwa ni siri kati yenu nyinyi wawili, siwezi nikayaweka kwenye beti za nyimbo."

Tazama video kamili hapo chini.