Jumatano , 4th Mei , 2016

Baraza la Madiwani manispaa ya Moshi limempa muda wa mwezi mmoja na nusu Mkurugenzi wa manispaa hiyo Jeshi Lupembe, kufuatilia la ununuzi wa eneo la makaburi lilipo kaika kijiji cha Mtakuja wilaya ya Moshi vijijini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, Jeshi Lupembe.

Wakizungumza katika kikao cha lawaida baadhi ya madiwani wamesema hawajaridhika na mchakato huo hivyo wameombwa kusimamishwa kwa malipo yaliyosalia ambapo manispaa imeshalipia shilingi milioni 40 kati ya milioni 42.

Madiwani hao wamesema baada ya kukaa kama kamati katika kikao cha wamebaini makosa mengi katika uandishi, hivyo wametoa mwezi na nusu wawe wamepata urekenbishaji wa hilo kashabrasha kisha watatoa kauli.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Jeshi Lupembe, amezungumzia suala hilo na kusema waliamua kutafuta eneo hilo nje ya mjini kutokana na uhaba wa ardhi unaoikabili masnipaa hiyo.

Aidha ameongeza kuwa lazima waangalie mchakato wa ununuzi ulifanyika pamoja na muhusika lakipi pia watathimi thaman ya eneo hilo kama lina uhalali wa kulipia fedha hizo katika eneo hilo.