Jumatano , 7th Dec , 2022

Jeshi la Polisi Lindi limewataka madereva kuwa makini barabarani ili kujiepusha na ajali hasa katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu za krismasi na mwaka mpya

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Lindi Kamishna Msaidizi Pilly Mande  amesisitiza Jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa magari kwa kushirikiana na madereva ili kuhakikisha abiria wapo kwenye vyombo salama huku akitoa takwimu ya makossa ya usalama barabarani mkoani Lindi kuwa 3273 kwa mwaka 2021/2022.

Kamishna Pilly Mande anasema, abiria husafiri ili wafike wanapoelekea salama na hasa katika msimu huu hutembelea sehemu mbalimbali kusherehekea sikukuu na si matarajio yao kupata ajali ambazo mara kadhaa huwa zinasababishwa na uzembe wa madereva.

Aidha, akizungumza na wanahabari ofisini kwake amekiri kuwepo kwa matukio ya uhalifu kama umiliki wa silaha, kesi za mauaji, uuzaji wa dawa za kulevya na pombe haramu na wizi wa nyara za serikali kama nyaya za umeme