
Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya El Niño na mabadiliko ya tabianchi, Balozi Macharia Kamau.
Hayo ni kwa mujibu wa Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya El Niño na mabadiliko ya tabia nchi, Balozi Macharia Kamau.
Balozi Kamau akizungumza na idhaa hii amesema nchi kama vile Msumbiji na Botswana zinakabiliwa na hali ngumu ya ukame huku njaa ikishuhudiwa miongoni mwa watu na wanyama wakifa.
Balozi Kamau ameongeza kwamba kufikia sasa Umoja wa Mataifa umepokea nusu tu ya ombi la ufadhili kwa ajili ya kukabiliana na madhara hayo na hivyo nchi hizo zinahitaji usaidizi zaidi kutoka nchi wahisani.