
Jamal Malizi (kushoto) na washtakiwa wenzake
Hayo yameelezwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri baada ya kesi hiyo kuitishwa leo kwa ajili ya kutajwa.
Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi January 16, 17 na 21, 2019 kwa ajili ya kuendelea na ushahidi, ikiwa imefikia shahidi wa 10.
Washitakiwa wengine ni Katibu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mhasibu wa shirikisho hilo, Nsiande Mwanga ambao wanakabiliwa na mashitaka 28, ikiwemo ya utakatishaji fedha ambazo ni Dola za Marekani, 375,418.
Baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, Malinzi na wenzake walipata wasaha wa kuwatakia kheri ya mwaka mpya, ndugu, jamaa na rafiki waliofika katika kesi yao.
Viongozi hao walishitakiwa muda mfupi kabla ya Uchaguzi Mkuu wa shirikisho hilo ambao ulifanyika Agosti, 2017 na nafasi ya Urais ikichukuliwa na Wallace Karia.