
Wananchi wa kijiji cha Chimati wakiwa na mkuu wa wilaya ya Nyasa Mh. Isabela Chilumba
Wakiongea wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi huo ulio kamilika kwa asilimia 85 na kugharimu kiasi cha shilingi milioni 356, wananchi wa kijiji cha Chimati kilichopo wilaya ya Nyasa mkoa wa Ruvuma wamesema walikuwa wanapata kero kubwa ya upatikanaji wa maji safi na salama.
''Tulikuwa tunapata taabu kufuata maji mbali hali iliyokuwa inasababisha ndoa nyingi kuvunjika. Tunaishukuru serikali kwa mradi huu ambao unaondoa kero hiyo kubwa'', amesema Amos Mbemba mkazi wa kijiji cha Chimati.
Kufuatia mradi huo kuanza kutoa maji katika kijiji hicho lakini matunzo ya mradi huo kwa wananchi yamekua mabovu hali hiyo ikamsikitisha mkuu wa wilaya ya Nyasa Mh. Isabela Chilumba na amewataka wananchi hao kutunza miradi ambayo serikali inaileta kwa ajili yao.