Majibu ya Fid Q kuhusu picha yake na Nandy

Jumanne , 15th Oct , 2019

Kupitia EATV & EA Radio Digital, Mkongwe wa muziki wa HipHop Bongo Fid Q, amenyoosha maelezo kuhusu picha iliyosambaa na kuzua taharuki katika mitandao ya kijamii ikimuonesha amesimama na Nandy.

Kwanza yale yalikuwa mambo ya upepo, nilishangaa kwa sababu mambo ya walimwengu niliipokea kama ya walimwengu kwahiyo sio 'issue', Mke wangu Mama Cheusi hakutoa maoni yoyote kuhusiana na ile picha ni kama hajaiona bado” amesema Fid Q.

Pia msanii huyo ameongelea suala la watu wengi kutegemea sana mitandao ya kijamii kama kuzusha habari, kupata umbea au kufuatilia maisha ya mtu.

Ni hatua ambayo ilibidi tufike lakini wasiwasi wangu ni mapokeo ya wengi yamekuwa si sawa sana kwa sababu wengi wanatumia huko kuwaumiza watu kwa kusemwa , kutukanwa , kusimangwa ndiyo maendeleo hayo yanakuja hivyo mengine kwa njia ya hasi mengine kwa njia ya chanya kwa sisi wasanii, tunaichukulia kama sehemu ya kujitangaza na zaidi imetupa nguvu ya kujiwezesha kama kutokuwa watumwa wa vyombo vya habari” ameongeza.

Aidha amesema kuna tofauti kati ya maisha yake binafsi ambayo ni siri na yale ambayo yapo mbele za watu.