Ijumaa , 25th Nov , 2022

Taarifa kutoka shirika la kupambana na ufisadi nchini Malawi zinasema kwamba polisi nchi hiyo wanamshikilia  makamu wa rais wa nchi hiyo kufuatia madai ya rushwa.

Kiongozi huyo wa ngazi ya juu Bw.Saulos Chilima anatuhumiwa kupokea dola zakimarekani  280,000 amabzo ni sawa na zaidi ya shilingi milioni 654  kutoka kwa mfanyabiashara ili kusaidia kupata tenda za serikali.

  Anatarajiwa kupandishwa mahakamani ambako atakabiliwa na mashtaka sita yanayohusiana na ufisadi, shirika hilo limesema.

Bw Chilima bado hajazungumzia madai hayo, lakini tovuti moja ya habari nchini humo imesambaza picha yake akiwasili mahakamani katika mji mkuu wa Lilongwe.