Jumatatu , 23rd Jun , 2014

Bodi ya huduma za maktaba nchini Tanzania imetakiwa kusogeza huduma zake karibu na wananchi hususani zile zinazohusiana na elimu pamoja na maarifa ya namna ya kupambana na umaskini.

Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Dkt Shukuru Kawambwa.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bi. Consolata Mgimba amesema hayo leo jijini Dar-es-Salaam wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya wakurugenzi ya huduma za maktaba.

Bi. Mgimba ametaja baadhi ya maarifa hayo kuwa ni jinsi jamii inavyoweza kuongeza uzalishaji mashambani, kujikinga dhidi ya magonjwa na hata mbinu za kuchochea kasi ya ukuaji wa Uchumi.